BRI yaleta muunganisho ulioimarishwa kwa maendeleo na ustawi wa pamoja: wataalam

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2023
BRI yaleta muunganisho ulioimarishwa kwa maendeleo na ustawi wa pamoja: wataalam
Picha hii ya angani iliyopigwa Aprili 26, 2023 ikionyesha eneo la ujenzi wa Reli Kiunganishi ya Pwani ya Mashariki (ECRL), mradi mkubwa wa miundombinu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) mjini Kelantan, Malaysia. (Xinhua/Zhu Wei)

KUALA LUMPUR – Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililotolewa na China limesonga mbele muongo mmoja tangu kuzinduliwa kwake na linaendelea kukua katika wigo na kiwango, na kuleta muunganisho bora wa miundombinu kwa maendeleo na ustawi wa pamoja, wataalam wamesema kwenye kongamano la kimataifa lililofanyika Kuala Lumpur, Malaysia.

Kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kimataifa la Asia Mpya Jumuishi (IFNIA) 2023 siku ya Jumatatu, Ong Tee Keat, Mkuu wa Taasisi ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja ya Asia Pasifiki ametoahotuba akisifu mafanikio madhubuti yaliyofikiwa na BRI katika muongo mmoja uliopita.

Tangu ilipotolewa Mwaka 2013, BRI imekua na kujumuisha miradi zaidi ya 3,000 katika nchi na kanda 152 na imeleta mabadiliko makubwa katika mageuzi ya uwezo wa ushindani wa kiuchumi kwa nchi washirika, huku utafiti wa Benki ya Dunia wa Mwaka 2019 ukiripoti kuwa BRI inatarajiwa kuongeza mapato halisi kati ya asilimia 1.2 na 3.4 kwa nchi zinazoshiriki, Ong amesema.

“Miradi ya uchukuzi ya BRI inaweza kupunguza muda wa kusafiri kwenye kanda za kiuchumi kwa asilimia 12, kuongeza biashara kati ya asilimia 2.7 na 9.7, na kuondoa watu milioni 7.6 kutoka kwenye umaskini uliokithiri,” amesema.

Lin Shiguang, Konsela wa Ubalozi wa China nchini Malaysia, amesema katika hotuba yake kwamba ushirikiano wa BRI unatoa suluhisho za China kwa ustawi wa dunia, akitaja njia za reli zenye mafanikio zilizojengwa Laos na Indonesia na ujenzi unaoendelea wa Reli Kiunganishi ya Pwani ya Mashariki (ECRL) nchini Malaysia, ambazo zimeboresha muunganisho na kuongeza shughuli za kiuchumi.

"Hebu tuendeleze maendeleo ya kisasa kwa nchi zote, tujenge Dunia iliyo wazi, jumuishi na iliyounganishwa kwa maendeleo ya pamoja, na tujenge kwa pamoja jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu," amesema.

Kwa upande wake, Seneta na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi ya Bunge la Seneti ya Pakistan, Mushahid Hussain Syed, katika hotuba yake kwa njia ya video, amesema China leo ndiyo nchi inayoongoza kwa utandawazi, kutokana na historia yake ndefu ya biashara na mitandao inayoanzia kwenye Njia ya Kale ya Hariri.

“Juhudi za maendeleo na ushiriki wa China duniani kupitia BRI pamoja na kustawi kwake kiuchumi kwa njia ya amani kumeiweka kipekee kuwa kielelezo mbadala cha maendeleo,” amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha