Eneo la kwanza duniani la Zootopia laanza uendeshaji wa majaribio kwenye Bustani ya Disney mjini Shanghai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2023
Eneo la kwanza duniani la Zootopia laanza uendeshaji wa majaribio kwenye Bustani ya Disney mjini Shanghai
Picha hii iliyopigwa Novemba 29, 2023 ikionyesha modeli ya Chief Bogo kwenye Eneo la Zootopia katika Bustani ya Starehe na Burudani ya Shanghai Disney, mjini Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Ren Long)

SHANGHAI - Eneo la kwanza duniani lenye mandhari maalum ya Zootopia, lililopangwa kufunguliwa kwa umma kuanzia Desemba 20 mwaka huu kwenye Bustani ya Starehe na Burudani ya Shanghai Disney limeanza uendeshaji wa majaribio, bustani hiyo ya mapumziko imesema Jumatano.

Eneo hilo jipya lilifunguliwa kwa vyombo vya habari kwa mara ya kwanza Jumatano. Linatokana na jina la filamu maarufu ya katuni iliyozalishwa na Disney ya Zootopia pia litakuwa eneo la nane la mandhari ndani ya bustani hiyo.

Kwa mujibu wa eneo hilo la mapumziko, ujenzi wa eneo hilo la Zootopia ulianza Desemba 2019, na unajumuisha dhana nyingi za hivi karibuni za muundo kutoka kwa timu ya kimataifa ya uhandisi ya Disney.

Bustani ya Starehe na Burudani ya Shanghai Disney ilifunguliwa kwa umma ikiwa na maeneo sita yenye mandhari mbalimbali Juni 16, 2016. Eneo lake la saba, Disney Pixar Toy Story, lilifunguliwa Mwaka 2018, na kuifanya Shanghai Disney kuwa bustani inayopanuka kwa haraka zaidi duniani. Mwezi Agosti mwaka huu, bustani hiyo ilianza ujenzi wa hoteli yake ya tatu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha