Mkutano wa Tabianchi wa COP28 watoa wito wa kuharakisha mwitikio wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi duniani (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 01, 2023
Mkutano wa Tabianchi wa COP28 watoa wito wa kuharakisha mwitikio wa kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi duniani
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi akihutubia ufunguzi wa Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, Novemba 30, 2023. (Xinhua/ Wang Dongzhen)

DUBAI – Mkutano wa 28 wa Nchi Watia saini wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN) wa Mabadiliko ya Tabianchi, umeanza Alhamisi alasiri mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu na umevutia umakini wa kimataifa wakati unapoadhimisha hitimisho la Hatua za Kimataifa (Global Stocktake), ambayo ni tathmini ya kwanza kabisa ya miaka miwili ya maendeleo ya pamoja ya dunia kuelekea malengo ya Makubaliano ya Paris ya 2015.

Baada ya kuteuliwa rasmi kuwa mwenyekiti wa COP28, Sultan Ahmed Al Jaber amesema "barabara mpya inaanza na uamuzi kuhusu Hatua za Kimataifa, uamuzi ambao ni kabambe, unaorekebisha mwenendo na kuharakisha hatua hadi 2030."

Al Jaber ametoa wito wa uungaji mkono kwa viongozi wa dunia, akiwahimiza kufanya vitendo vya haraka kuhusu Hatua za Kimataifa, kufikia makubaliano ya haraka juu ya ajenda, na kutekeleza hatua za haraka katika makubaliano.

Ameeleza kuwa "nchi mwenyekiti wa mkutano wa awamu hii imejitolea kufungua ufadhili wa kifedha (wa kijani) ili kuhakikisha kwamba nchi za Dunia ya Kusini hazitahitaji kuchagua kati ya maendeleo na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi," huku akitoa wito kwa pande zote kutafuta muafaka, kuja mbele na suluhu, na kufikia muafaka.

Kwenye ufunguzi wa mkutano, Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi, Simon Stiell amesema "tunapiga hatua dogo. Kupiga hatua kutoka kwa Dunia isiyo na utulivu inayokosa uhimilivu, tunatakiwa kutoa mwitikikio bora kwa kukabiliana na athari yenye utatanishi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini hatua tunayopiga ni ya polepole sana. "

Mkutano huo, ulioanza Novemba 30 na utaendelea hadi Desemba 12, ambao utakaribisha ujumbe wa watu zaidi ya 70,000 kutoka duniani kote katika jitihada za kutafuta suluhu ya dunia nzima kwa masuala mazito ya tabianchi yanayokabili sayari na binadamu wote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha