Rais Xi Jinping asisitiza kuharakisha ujenzi wa Shanghai kuwa mji mkubwa wa kisasa wa kimataifa wa kijamaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2023
Rais Xi Jinping asisitiza kuharakisha ujenzi wa Shanghai kuwa mji mkubwa wa kisasa wa kimataifa wa kijamaa
Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akikagua eneo la makazi ya watu wanaoishi kwenye nyumba za kupanga zinazofadhiliwa na serikali mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Novemba 28, 2023. (Xinhua/Shen Hong)

SHANGHAI/YANCHENG - Rais wa China Xi Jinping katika ziara ya ukaguzi mjini Shanghai iliyoanza Jumanne hadi Jumamosi amesisitiza haja ya kuharakisha ujenzi wa Shanghai kuwa mji mkubwa wa kisasa, wa kijamaa na wa kimataifa kwa kujikita zaidi katika ujenzi wa vituo vya kimataifa vya uchumi, mambo ya fedha, biashara, usafirishaji na uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia.

Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ameitaka Shanghai kuharakisha kujijenga na kuwa mji mkubwa wa kisasa, wa kijamaa na wa kimataifa wenye ushawishi wa kimataifa, na kutoa mchango mkubwa na wa kupigiwa mfano katika kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.

Wakati wa ukaguzi wake katika Soko la Biashara ya bidhaa za Baadaye la Shanghai (Shanghai Futures Exchange) siku ya Jumanne alasiri mara tu aliposhuka kwenye treni, maara tu alikwenda kukagua soko hilo, Rais Xi amehimiza soko hilo kuharakisha ujenzi wa soko la kimataifa la kiwango cha juu, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya utafiti wa ujenzi wa mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa biashara ya bidhaa za baadaye zenye sifa maalumu ya China na kujenga kituo cha kimataifa cha mambo ya fedha.

Alipotembelea Mji wa Sayansi wa Zhangjiang katika Eneo Jipya la Pudong, Rais Xi amesema kusukuma mbele maendeleo ya mambo ya kisasa ya China hakuwezi kutenganishwa na uungaji mkono wa kimkakati wa sayansi na teknolojia, elimu na vipaji, na kwamba Shanghai inapaswa kuongoza katika suala hili.

Siku ya Jumatano alasiri, Rais Xi alitembelea jumuiya ya makazi katika Wilaya ya Minhang ambayo imejitolea kujenga nyumba za kupanga za bei nafuu kwa wakazi wapya wa mijini, vijana na wafanyakazi wa mstari wa mbele.

Rais Xi amesema amefurahi kuona wajenzi wa mji wa Shanghai kutoka kote nchini China wakiishi na kufanya kazi hapa kwa furaha na kuridhika. Amesema, wafanyakazi wahamiaji wanaotoa mchango katika Mji wa Shanghai pia ni mabwana wa mji huo.

Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais Xi alifahamishwa kuhusu kazi ya mji huo inayofanywa na Kamati kuu ya CPC na serikali ya mji wa Shanghai.

Rais Xi amesisitiza kuweka mazingira ya biashara yenye kiwango cha kimataifa, akisema kuwa Shanghai inapaswa kupiga hatua kwenye kiwango cha juu katika kuendeleza kwa kina na kwa pande zote mageuzi na kufungua mlango, amehimiza mji huo kutoa nguvu kubwa zaidi katika kuendeleza mfano wake anzilishi wa mageuzi na ufunguaji mlango katika sekta zote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha