

Lugha Nyingine
Viti vya magurudumu na magongo hayawezi kuzuia ndoto: Simulizi za walemavu wanaojishughulisha kwa bidii huko Lhasa, China
![]() |
Juelie (wa tano kulia mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi mbele ya shirika aliloanzisha (Picha ya tarehe 1, Desemba). |
Katika Mji wa Lhasa ulioko Mkoa wa Xizang nchini China, kuna kundi la vijana. Ingawa vijana hawa ni walemavu, wamekuwa wakijishughulisha kwa bidii sana kutimiza ndoto zao na kuishi katika maisha yao bora hapa duniani.
Juelie mwenye umri wa miaka 36 ni “mjasiriamali nyota” kati ya vijana hao. Ajali iliyotokea mnamo mwaka 2009, ilimwacha akiwa ameshikamana na kiti cha magurudumu. Baada ya muda wa mfadhaiko, chini ya msaada wa familia na jamii, Juelie alianzisha biashara yake mwenyewe. Hadi hivi sasa kampuni ya Juelie ina waajiriwa 42, miongoni mwao 27 ni walemavu.
Juelie pia ni nyota wa timu ya mpira wa kikapu wa viti vya magurudumu ya mji wa Lhasa. Mwaka 2021 alipocheza kwenye mchezo ulioandaliwa na Kituo cha Kuhudumia Watu wenye Ulemavu cha Lhasa, alijipatia shabiki wake mkubwa aitwaye Lhakpa Dhundrup. Lhakpa Dhundrup mwenye umri wa miaka 22 alikuwa amepata mivunjiko kadhaa ya mifupa tangu alipokuwa mtoto mchanga na aliwahi kuugua ugonjwa wa “mifupa ya kaukau”. Sasa akiwa mtu mzima hawezi kutembea bila ya kutegemea magongo na kiti cha magurudumu kinachotumia umeme. Hata hivyo, ugonjwa na bahati mbaya yake ya kimaumbile haimkatishi tamaa. Alishika kamera na kuwa na ndoto ya kuwa mpiga picha. Hivi sasa Lhakpa Dhundrup ameondoka Kituo cha Kuhudumia Watu wenye Ulemavu na kufanya kazi ya upigaji picha na utengenezaji video kwenye kampuni ya Juelie na kuanzisha maisha ya kujitegemea.
Dolkar, msichana wa Lhasa mwenye umri wa miaka 29 alipata ulemavu kwa sababu ya ugonjwa wa polio. Dolkar alijifunza kaligrafia ya lugha ya Kitibeti katika kampuni ya Juelie, akawa mwendeshaji wa darasa la kaligrafia ya Kitibeti na ala ya muziki ya Kitibeti sgra snyan. Kwa idadi ya juu, wanafunzi wa darasa lake walifikia 150. Hivi sasa mshahara wake wa kila mwezi unafikia Yuan 9,000 hivi (takriban Dola za Kimarekani 1272.63) kabla ya kutozwa kodi.
Wakati wa mchakato wa kuanzisha ujasiriamali wake, Shirikisho la Walemavu la Mji wa Lhasa lilimfadhili Juelie Yuan 420,000 (sawa na Dola za Marekani 59,389); Shirikisho la Walemavu la Mkoa unaojiendesha wa Xizang pia limeisaidia shirika lake kufunga lifti bila ya vizuizi.
Picha na Jiang Fan/Xinhua
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma