

Lugha Nyingine
Israel yaanzisha mashambulizi ya anga huko Gaza, makumi ya watu wauawa (7)
![]() |
Watu wakiomboleza vifo vya watu waliouawa kwenye mashambulizi ya anga ya Israel katika Mji wa Deir el-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 3, 2023. (Xinhua) |
GAZA - Wizara ya Afya inayoongozwa na Kundi la Hamas imesema kuwa Israel imeanzisha mashambulizi mapya ya anga katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza siku ya Jumapili, na kusababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa.
Wafanyakazi wa uokoaji na matabibu wameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba mashambulizi hayo ya anga ya Israel yalilenga jengo la makazi linalokaliwa na watu wa familia ya Abu Aita katika Kambi ya Jabalia iliyoko Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza ambapo watu thelathini na saba wameuawa na kuhamishiwa hospitalini katika muda wa saa chache zilizopita.
Wakati huo huo, watu takriban watatu wameuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika mashambulizi ya makombora ya Israel yaliyolenga nyumba inayomilikiwa na familia ya Abu Jiyab katika eneo la Abu Eskandar, kaskazini mwa Mji wa Gaza, kwa mujibu wa watoa huduma za matabibu.
Aidha, idara ya ulinzi wa raia ya Palestina imesema kuwa watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika nyumba zilizobomolewa kwa ndege za kivita za Israel kwenye Mtaa wa Yafa, Mashariki mwa Mji wa Gaza.
Mapema siku hiyo, msemaji wa idara hiyo, Mahmoud Basal alisema kuwa watu 84 waliofariki walikuwa wamepelekwa hospitali ya Al-Muamalat huko Gaza kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel katika saa chache zilizopita.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Vyombo vya Habari ya serikali ya Palestine, Ismael Al-Thawabteh amewaambia waandishi wa habari Jumapili kwamba Wapalestina zaidi ya 700 wameuawa huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma