China yaisaidia Misri kurusha satelaiti mpya kuingia kwenye obiti katika anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2023
China yaisaidia Misri kurusha satelaiti mpya kuingia kwenye obiti katika anga ya juu
Roketi ya kubeba satelaiti kwenda anga ya juu ya Long Mardh-2C iliyobeba satelaiti ya MISRSAT-2 ikiruka kutoka Kituo cha Urushaji wa Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China Desemba 4, 2023. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)

China imeisaidia Misri kurusha satelaiti ya kuhisi kutoka mbali kuingia kwenye obiti katika anga ya juu kutoka Kituo cha Urushaji wa Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini Magharibi mwa China siku ya Jumatatu wiki hii.

Satelaiti hiyo inayoitwa MISRSAT-2 iliyorushwa na roketi ya kubeba satelaiti kwenda anga ya juu ya Long March-2C saa 6:10 mchana (kwa saa za Beijing), itatumiwa na Misri katika matumizi ya ardhi na maliasili, uhifadhi wa maji, kilimo na nyanja nyingine.

MISRSAT-2 ni mradi kinara wa ushirikiano wa kina kati ya China na Misri katika nyanja ya teknolojia ya hali ya juu ya anga ya juu, limesema Shirika la Taifa la anga ya juu la China (CNSA).

Hii ni safari ya 499 ya roketi za mfululizo wa Long March kwenda anga ya juu. Satelaiti za kuhisi kutoka mbali za Starpool 02-A na Starpool 02-B pia zimerushwa kwenda anga ya juu wakati huohuo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha