Balozi wa Palestina asema Palestina inaishukuru China kwa kupeleka msaada kwa watu wa Gaza katika wakati wa uhitaji (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2023
Balozi wa Palestina asema Palestina inaishukuru China kwa kupeleka msaada kwa watu wa Gaza katika wakati wa uhitaji
Lori lililobeba msaada wa kibinadamu uliotolewa na China kwa Ukanda wa Gaza kupitia Misri likionekana huko Cairo, Misri tarehe 27, Novemba, 2023. (Xinhua/Sui Xiankai)

Balozi wa Palestina nchini Misri Diab al-Louh amewasilisha shukrani za dhati za nchi yake kwa serikali na watu wa China kwa kutoa kwa wakati msaada wa kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza unaokumbwa na vita.

Diab al-Louh alisema hayo kwenye hafla iliyofanyika siku ya Jumapili mjini Cairo, Misri kwa ajili ya kuadhimisha juhudi ya China ya kutoa msaada, ambayo pia ilihudhuriwa na Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mwezi Mwandamo Mwekundu la Misri Rami Al-Nazer.

Balozi wa China amesema kuwa, China imesafirisha kwa meli malori manane yenye kubeba vitu vya msaada, vikiwemo makopo, biskuti, maziwa, asali, na maji ya kunywa kwenye Mji wa Arish wa Misri, ambavyo baadaye vitapelekwa kwenye eneo hilo lililodhibitiwa la pwani la Gaza kwa kupitia kituo cha kuvuka mpaka cha Rafah, ambacho huonwa kama njia ya maisha na watu wa Gaza.

Liao pia ametoa shukrani kwa msaada wa Shirika la Mwezi Mwandamo Mwekundu la Misri.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha