Wawakilishi wa ujumbe mbalimbali kwenye Mkutano wa COP28 watoa wito wa kukusanya hekima na nguvu ili kuendeleza mageuzi ya nishati mbadala duniani (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2023
Wawakilishi wa ujumbe mbalimbali kwenye Mkutano wa COP28 watoa wito wa kukusanya hekima na nguvu ili kuendeleza mageuzi ya nishati mbadala duniani
Xin Baoan, Mkuu wa Shirika la Maendeleo na Ushirikiano wa Nishati Duniani (GEIDCO) na Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Gridi la Taifa la China, akizungumza kwenye mkutano wa nishati mjini Dubai, Falme za Kiarabu, Desemba 5, 2023. (Xinhua/ Wang Dongzhen)

DUBAI – Wawakilishi kutoka ujumbe zaidi 70 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi wamekutana siku ya Jumanne mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, kutafuta maarifa na suluhu kwa ajili ya mageuzi yaliyo jumuishi, ya haki na yenye uhimilivu katika matumizi ya nishati mbadala duniani.

Mkutano huo wa nishati umekufanyika wakati ambapo mazungumzo ya tabianchi kwenye mkutano wa COP28, au Mkutano wa 28 wa Nchi watia saini kwenye Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC), yakiwa yamekwama kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na mageuzi ya nishati mbadala.

Wajumbe wanaohudhuria mkutano huo, wakiwemo mjumbe maalum wa masuala ya tabianchi wa China, maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, na maafisa wa nishati wa Misri na Malawi, walikutana pembezoni mwa mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa tabianchi unaoendelea na walitoa mwito wa kukusanya hekima na nguvu zaidi ili kuendeleza mageuzi ya nishati mbadala duniani.

"Tuko katika wakati muhimu wa safari yetu ya pamoja kuelekea kwenye matumizi ya nishati mbadala ulio wa haki na jumuishi. Ni dhahiri kwamba kazi hii kubwa haiwezi kufikiwa na shirika au taifa lolote peke yake," amesema Rola Dashti, Katibu Mtendaji wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi na Jamii ya Asia Magharibi (UNESCWA).

Amesisitiza kuwa, kwa juhudi za pamoja, sekta ya nishati inaweza "kubadili kutoka changamoto hadi suluhisho ili kufikia malengo ya tabianchi."

Akihutubia mkutano huo, mjumbe maalum wa China kuhusu mabadiliko ya tabianchi Xie Zhenhua ameeleza matumaini yake kuwa hekima na nguvu vinaweza kuunganishwa ili kutafuta suluhu ya kuvuka mkwamo kuelekea malengo ya matumizi ya nishati mbadala. Ameongeza kuwa, inapaswa kuwa suluhisho la kivitendo na la mfano ambalo linaweza kuchangiwa na kuigwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha