Magari ya China yanayotumia umeme yahudumia Mkutano wa COP28 unaofanyika Dubai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 06, 2023
Magari ya China yanayotumia umeme yahudumia Mkutano wa COP28 unaofanyika Dubai
Gari dogo linalotumia umeme la kampuni ya magari ya China ya Guangdong Lvtong likitoa huduma kwa watembeleaji kwenye “eneo la kijani” la Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Dubai (COP28).

Tangu Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Dubai (COP28) ulipofunguliwa, magari yanayotumia umeme ya chapa za China, zikiwemo Higer na BYD yamekuwa yakitoa huduma ya mabasi ya kupeleka na kurudisha watu mkutanoni. Magari madogo 50 yanayotumia umeme ya kampuni ya magari ya Guangdong Lvtong ya China yamekuwa yakitoa huduma ya kupakia na kushusha watu katika vituo mbalimbali vya eneo la kijani la mkutano huo. Magari hayo yamekuwa yakileta mandhari ya kuvutia katika mkutano huo.

Picha na Wang Dongzhen/Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha