Mradi wa Uzalishaji Umeme kwa Upepo kupunguza utoaji wa kaboni mkoani Heilongjiang, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2023
Mradi wa Uzalishaji Umeme kwa Upepo kupunguza utoaji wa kaboni mkoani Heilongjiang, China
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye sehemu ya ujenzi ya kituo cha uzalishaji umeme kwa upepo katika Wilaya ya Yilan, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Jianwei)

Mkoa wa Heilongjiang ulioko Kaskazini zaidi mwa China kwa sasa umefunikwa na barafu na theluji, lakini ujenzi na uendeshaji wa sehemu ya nne ya mradi wa kituo cha uzalishaji umeme kwa upepo wenye uwezo wa Megawati 200 kwa namna yoyote “haujaganda”.

Mradi huo unalenga kufunga mitambo 32 ya uzalishaji umeme kwa upepo, ambayo kila mmoja una uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 6.25. Shehena ya kwanza ya mitambo hiyo imeunganishwa kwenye gridi ya taifa kwa ajili ya uzalishaji umeme tarehe 28, Novemba.

Itakapoanza kufanya kazi kikamilifu, mitambo hiyo ya sehemu ya nne ya mradi huo inatarajiwa kuingiza umeme wa kilowati milioni 570 kwa saa kila mwaka kwa gridi, ambayo ni sawa na kuokoa matumizi ya makaa sanifu yenye uzito wa tani 169,000, na pia ni sawa na kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni kwa tani 462,000.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha