Ubalozi wa China watoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi maskini wa Misri (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2023
Ubalozi wa China watoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi maskini wa Misri
Wanafunzi wakitazama mabegi na vifaa vya shule kwenye hafla ya kutoa misaada iliyofanyika katika kituo cha huduma cha Wilaya ya Al-Asmarat katika Jimbo la Cairo, Misri, Desemba 5, 2023. (Xinhua/Sui Xiankai)

CAIRO - Ubalozi wa China nchini Misri, kwa kushirikiana na chama tawala cha Misri cha Homat Al Watan (Walinzi wa Taifa), siku ya Jumanne katika hafla ya kutoa misaada iliyofanyika kwenye kituo cha huduma cha Wilaya ya Al-Asmarat katika Jimbo la Cairo umetoa vifaa vya shule kwa wanafunzi maskini ambavyo vinajumuisha seti takriban 400 za mabegi na vifaa vya shule.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang, Katibu Mkuu wa chama cha Homat Al Watan cha Misri Tariq Naseer na Mkuu wa Wilaya ya Al-Asmarat Ahmed Ibrahim.

Katika hafla hiyo, Balozi Liao amesema msaada huo unalenga kuonesha uungaji mkono kwa mradi wa ukarabati wa mtaa wa makazi duni uliozinduliwa na Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi, na kuongeza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Nasser ametoa shukrani za chama chake kwa upande wa China kusaidia miradi ya kuboresha shughuli za maisha ya watu wa Misri. Amesema, msaada huo unaonyesha urafiki kati ya Misri na China.

Akitoa shukurani kwa ubalozi wa China, Ibrahim amesema wilaya yake ilizindua mradi wa kwanza wa ukarabati wa mtaa wa makazi duni chini ya Mpango wa Maisha yenye Hadhi uliotolewa na rais Sisi.

Mradi huo ulizinduliwa Mwaka 2019 ili kutoa maisha yenye hadhi kwa watu wanaoishi katika mazingira hatarinishi kote nchini humo. Pia unchangia katika kuimarisha ubora wa huduma za kila siku za umma zinazotolewa kwa wananchi, pamoja na wakazi wa maeneo ya vijijini.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha