Kituo kipya cha utafiti wa kisayansi kuanzishwa kando ya maeneo ya pwani ya Bahari ya Ross

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2023
Kituo kipya cha utafiti wa kisayansi kuanzishwa kando ya maeneo ya pwani ya Bahari ya Ross
Wataalam wa Kundi la 40 la Utafiti wa Kisayansi katika Bahari ya Antaktika la China wakijiandaa kupakua mashine karibu na maeneo ya pwani ya Bahari ya Ross, Desemba 7, 2023. (Xinhua/Zhou Yuan)

Kituo kipya cha utafiti wa kisayansi kitaanzishwa kwenye maeneo ya pwani ya Bahari ya Ross wakati wa safari hii ya kitafiti ya Kundi la 40 la Utafiti wa Kisayansi katika Bahari ya Antaktika la China, na kuwa kituo cha tano cha China cha utafiti katika Bahari ya Antaktika na cha tatu cha kudumu, baada ya vituo vya awali vya Changcheng na Zhongshan. Meli ya utafiti ya China ya kupasua barafu, Xuelong 2 na meli ya mizigo Tian Hui zimefika karibu na maeneo ya pwani siku ya Jumatano. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha