China na Singapore zakubaliana kuboresha makubaliano ya kibiashara, mpango wa kuondoleana hitaji la visa kwa siku 30 (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2023
China na Singapore zakubaliana kuboresha makubaliano ya kibiashara, mpango wa kuondoleana hitaji la visa kwa siku 30
Ding Xuexiang, Naibu Waziri Mkuu wa China akihudhuria kwa pamoja na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Singapore Lawrence Wong hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Eneo la Uvumbuzi wa Kijani la Kituo cha Mji wa kiikolojia wa China na Singapore wa Tianjin mjini Tianjin, Kaskazini mwa China, Desemba 7, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

TIANJIN - China na Singapore zimetangaza siku ya Alhamisi kwamba zimefikia makubaliano ya kuboresha zaidi Mkataba wa Biashara Huria kati ya China na Singapore (CSFTA), huku pia zikikubaliana juu ya mpango wa kuondoleana hitaji la visa kwa siku 30 kwa raia wa nchi hizo wanaotumia pasipoti za kawaida kwenye mkutano kati ya Ding Xuexiang, Naibu Waziri Mkuu wa China na Lawrence Wong, Naibu Waziri Mkuu na ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Singapore mjini Tianjin.

Ding na Wong pia wameshiriki mkutano wa 19 wa Baraza la Pamoja la Ushirikiano wa Pande mbili kati ya China na Singapore, mkutano wa 24 wa Baraza la Uendeshaji wa Pamoja wa Eneo maalum la Viwanda la Suzhou (JSC), mkutano wa 15 wa Mji wa Kiikolojia wa China na Singapore wa Tianjin JSC na mkutano wa saba wa Mradi Kielelezo wa China na Singapore (Chongqing) kuhusu Muunganisho wa Kimkakati JSC.

Ding amesema mwaka huu ni wenye umuhimu wa pekee kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Singapore. Amezitaka pande hizo mbili kuzingatia kwa karibu mwelekeo mpya wa uhusiano kati ya China na Singapore, kutumia vyema jukwaa la mkutano wa utaratibu wa ushirikiano wa pande mbili, kuhimiza uboreshaji wa ushirikiano uliopo, kutafuta fursa mpya zaidi za ushirikiano, na kutekeleza kwa pamoja makubaliano muhimu ya viongozi wa nchi hizo mbili.

“Uhusiano kati ya Singapore na China unaendelezwa kwa kasi, na Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja limepata matokeo mazuri” Wong amesema, huku akiongeza kuwa Singapore iko tayari kushirikiana na China ili kuimarisha zaidi mabadilishano katika ngazi zote, kuimarisha ushirikiano wa mikakati ya maendeleo, kutoa nafasi kubwa kwa mchango wa utaratibu wa ushirikiano wa pande mbili na kuhimiza uhusiano wa pande mbili kupata maendeleo mapya.

Pande hizo mbili zimekubaliana kuongeza ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, kuendelea kupanua na kuimarisha ujenzi wa Ukanda Mpya wa Kimataifa wa Biashara ya Nchi kavu na Baharini, kuimarisha ushirikiano katika masoko ya upande wa tatu, kuboresha miradi muhimu ya ushirikiano, kupanua kikamilifu ushirikiano katika uchumi wa kidijitali na nishati ya baharini, kuunda muundo wa mabadilishano ya kitamaduni na kati ya watu yaliyo anuai na yenye mchangamano, na kudumisha kwa pamoja mfumo wa biashara wa pande nyingi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha