Mageuzi ya reli ya Kenya yachochea maendeleo ya kisasa ya nchi hiyo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2023
Mageuzi ya reli ya Kenya yachochea maendeleo ya kisasa ya nchi hiyo
Picha iliyopigwa Novemba 27, 2023 ikionyesha mfano wa awali wa kichwa cha treni katika Jumba la Makumbusho ya Reli la Nairobi jijini Nairobi, Kenya. (Xinhua/Li Yahui)

NAIROBI - Jumba la Makumbusho ya Reli la Nairobi, lililo katika sehemu yenye shughuli nyingi za kibiashara mjini Nairobi, Kenya ambalo lina safu ya fasihi iliyohifadhiwa, mifano ya treni na reli zilizozeeka na hutumika kama msimulizi wazi wa mageuzi ya Kenya kutoka nchi koloni hadi nchi huru, likiendelea kuwa eneo maarufu kwa wenyeji na watalii wanaotamani kuzama katika historia tajiri ya Kenya.

Sevily Mwailemi, dereva wa treni mwenye umri wa miaka 58 ambaye alikuwa na uzoefu wa zaidi ya miongo mitatu, amesisitiza mchango muhimu wa historia ya Kenya unaofungamana na miundombinu yake ya reli.

Reli ya kwanza nyembamba kutoka mji wa bandari wa Mombasa hadi nyanda za juu, na kuishia kwenye mpaka wa Uganda, ilijengwa na wakoloni wa Uingereza kuanzia Mwaka 1896 hadi karibu 1901. Ikiwa ilipewa jina la "Nyoka wa Chuma," reli hiyo iliwezesha usafirishaji wa malighafi, ikiimarisha maslahi ya kiuchumi ya wakoloni wa Uingereza.

Baada ya Kenya kupata uhuru Mwaka 1963, reli hiyo nyembamba iliendelea na jukumu lake la usafirishaji wa mizigo na abiria. Na injini zinazotumia dizeli zilichukua mbadala wa injini za mvuke.

Hata hivyo, Mwailemi amesema urithi wa ukoloni unaoendelea kuwepo unahusishwa na reli hiyo ya zamani licha ya mchango wake katika maendeleo ya Kenya. Akiwa ameboresha ujuzi wake katika njia hii yenye historia kwa zaidi ya miongo mitatu, Mwaka 2021 alihamia hadi Reli ya Kisasa ya Mombasa-Nairobi (SGR) iliyojengwa kwa msaada wa China, ambayo amesema imechangia sehemu kubwa katika uchumi wa nchi hiyo.

"Naweza kusema SGR ni mradi mkubwa zaidi tangu uhuru. " Mwailemi amesema.

Ikiwa ilizinduliwa Mwaka 2017, reli hiyo ya SGR yenye urefu wa kilomita 472 ilipunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri na ikaibuka kuwa chaguo linalopendelewa na wasafiri, ikitoa mchango muhimu katika kuchochea biashara na kuwezesha ukuaji wa miji midogo kando ya reli hiyo.

Reli hiyo mpya ambayo mara nyingi hujulikana kama tunda la Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja, pia ni mradi mkuu wa mpango wa maendeleo wa muda mrefu wa Dira ya 2030 ya Kenya. Imefanya kazi bila kupumzika kwa zaidi ya siku 2,300, ikisafirisha mamilioni ya abiria na tani za bidhaa, na kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha