Rais wa China afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV)

(CRI Online) Desemba 13, 2023
Rais wa China afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV)
Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong aliandaa hafla ya kumkaribisha Rais Xi Jinping wa China katika uwanja wa Ikulu mchana wa tarehe 12, Desemba. (Picha inatoka shirika la habari la China Xinhua)

Rais wa China Xi Jinping Jumanne amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha Vietnam (CPV) Nguyen Phu Trong huko Hanoi, Vietnam.

Katika mazungumzo hayo, Rais Xi amesema China inaunga mkono kithabiti Vietnam kuendelea kuhimiza mambo ya ujenzi ya kijamaa, na kwamba anaamini kuwa chini ya uongozi wa kamati Kuu ya CPV, chama na serikali ya Vietnam itakamilisha kwa mafanikio majukumu yote yaliyowekwa katika Mkutano Mkuu wa 13 wa Chama cha CPV, na kuweka msingi thabiti kwa ajili ya kutimiza malengo ya ujenzi wa chama na wa nchi hiyo.

Rais Xi pia amesisitiza kuwa angependa kushirikiana na Bw. Nguyen Phu Trong kutangaza hadhi mpya ya uhusiano kati ya vyama na serikali za China na Vietnam, na kujenga kwa pamoja Jumuiya ya China na Vietnam yenye Mustakabali wa Pamoja ambayo ina umuhimu wa kimkakati.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha