

Lugha Nyingine
Mkutano wa COP28 watoa maafikiano ya "kihistoria" ya kuharakisha hatua za Tabianchi (5)
DUBAI - Mwenyekiti wa Mkutano wa Tabianchi wa COP28 Sultan Ahmed Al Jaber ametangaza Jumatano kwamba pande zote kwenye mkutano wa kilele wa Tabianchi wa Umoja wa Mataifa zimefikia maafikiano ya mwisho juu ya makubaliano "ya kihistoria" ya Tabianchi akisema " ni mipango mfululizo iliyoimarishwa, iliyo ya uwiano, lakini bila mashaka hata kidogo, mipango hiyo inalenga kuharakisha hatua za Tabianchi. Ni Maafikiano ya UAE" .
Makubaliano hayo yameweka hatua mfululizo za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kuhusu, kuzoea mabadiliko ya tabianchi, kukusanya mitaji na kuwa na unyumbufu, pamoja na nishati ya visukuku.
Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa mipango hiyo ni "yenye uwiano ambayo inashughulikia utoaji wa hewa chafu, unaziba pengo la kuhimili, kufikiria upya mambo ya fedha ya dunia nzima , na kuleta matokeo katika masuala ya hasara na uharibifu," akibainisha kuwa mipango hiyo imeanzishwa kwenye msingi wa pamoja, inaimarishwa kwa kupitia ushirikiano wa jumuishi na kuimarishwa kwa kupitia ushirikiano. .
Al Jaber ameelezea imani yake kwamba hatua hizi zote muhimu zitasaidia kujenga Dunia nzuri zaidi, safi zaidi, na yenye ustawi mkubwa na usawa zaidi, akihimiza kuchukua hatua za lazima ili kuyafanya makubaliano haya kuwa vitendo halisi .
Pia, amesema mkutano huo umeleta mabadiliko ya dhana ambayo "ina uwezekano wa kuupanga upya uchumi wetu."
Akihutubia mkutano wa mwisho wa COP28, Zhao Yingmin, mkuu wa ujumbe wa China kwenye COP28 ambaye ni Naibu Waziri wa Ikolojia na Mazingira wa China, amepongeza kwamba COP28 imetoa mwelekeo wa jumla kwa awamu inayofuata ya hatua za tabianchi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma