

Lugha Nyingine
Rais Putin asema Uhusiano wa China na Russia ni muhimu kwa utulivu wa kimataifa
MOSCOW - Rais wa Russia Vladimir Putin amesema siku ya Alhamisi kwenye mkutano wake wa kila mwaka na waandishi wa habari kwamba uhusiano kati ya China na Russia unatoa mchango muhimu kwa ajili ya kudumisha utulivu wa kimataifa na kwamba "uhusiano wa Russia na China ni moja ya hakikisho muhimu la utulivu duniani," huku akiongeza kuwa kiwango cha mawasiliano kati ya nchi zote mbili ni ya "juu zaidi kuliko hapo kabla."
Rais Putin pia amesisitiza kuwa Russia na China zinapanua uhusiano wao katika maeneo mbalimbali, akisema nchi hizo mbili zinaendeleza uhusiano katika ujenzi wa miundombinu na nyanja ya teknolojia ya hali ya juu. "Na tutaendelea kufanya hivyo," ameongeza.
Amesema urafiki kati ya nchi hizo mbili "haulengi upande wowote" bali unalenga kuzinufaisha Russia na China.
Siku ya Alhamisi, Putin alifanya mkutano wake wa 18 wa kila mwaka na waandishi wa habari pamoja na kipindi cha maswali na majibu cha "Laini ya Moja kwa Moja" mjini Moscow. Waandishi wa habari na raia wa Russia waliuliza maswali juu ya mambo mbalimbali kuhusu sera za ndani na nje, pamoja na hali ya jumla ya kiuchumi, kisiasa na kijamii ya nchi hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma