

Lugha Nyingine
Kenya yaanzisha ujenzi wa Reli mpya ya usafiri wa umma ili kupunguza msongamano barabarani katika Mji Mkuu (4)
![]() |
Rais wa Kenya William Ruto (katikati, mbele) akishiriki kwenye hafla ya kuanzishwa kwa ujenzi wa Reli ya Riruta-Ngong katika Kaunti ya Kajiado, Kenya, Desemba 15, 2023. (Xinhua/Han Xu) |
Rais wa Kenya William Ruto amezindua ujenzi wa Reli ya Riruta-Ngong siku ya Ijumaa inayolenga kupunguza msongamano wa barabarani mjini Nairobi.
Ruto amesema kuwa, reli hiyo ya upana wa mita moja yenye urefu wa kilomita 12.5, ambayo itajengwa na kampuni ya Barabara na Daraja ya China (CRBC) tawi la Kenya, itaunganishwa na reli iliyopo kwenye eneo la makazi la kitongoji cha Riruta katika Kaunti ya Nairobi na kurefushwa hadi eneo la Ngong katika Kaunti ya Kajiado. Reli hiyo itapita vituo vya Riruta, Karen, Bulbul na Ngong.
“Reli hii mpya itakuwa na uwezo wa kusafirisha abiria 10,000 kila siku, kwa hivyo kupunguza msongamano kwenye barabara zetu,” amesema Ruto, huku akiongeza kuwa reli hiyo itakapokamilika, itapunguza kwa nusu gharama ya usafiri mjini na kuchangia kupunguza gharama ya maisha kwa jumla.
Jiao Xuxue, naibu meneja mkuu wa kampuni ya CRBC tawi la Kenya amesema kuwa, mradi huo unatazamiwa kukamilishwa katika muda wa miezi 12 ijayo, na kipindi chake cha dhamana ya dosari ni miezi 12. Ameongeza kuwa reli hiyo inatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa shinikizo la matumizi ya Barabara ya Ngong, ambayo ni korido muhimu ya usafiri mjini Nairobi, na pia kuongeza usafirishaji kwenye njia iliyopo ya reli ya upana wa mita moja mjini Nairobi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma