Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa DPRK Pak Myong Ho (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2023
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa DPRK Pak Myong Ho
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Pak Myong Ho mjini Beijing, China, Desemba 18, 2023. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) Pak Myong Ho siku ya Jumatatu mjini Beijing akisema urafiki wa jadi kati ya China na DPRK ni mali yenye thamani kwa pande zote mbili.

Katika miaka ya hivi karibuni, urafiki wa jadi kati ya China na DPRK umeendelezwa zaidi katika zama mpya chini ya mwongozo wa kimkakati na ufuatiliaji wa wakuu wa nchi hizo mbili, Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ameeleza.

Amesema China daima inautazama uhusiano kati yake na DPRK kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu na kuongeza kuwa, China iko tayari kushirikiana na DPRK ili kuimarisha mawasiliano na uratibu, na kuzidisha mabadilishano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande wake Pak amesema ni msimamo usioyumba wa upande wa DPRK kuendeleza kwa uendelevu uhusiano kati ya DPRK na China kwa mujibu wa nia ya wakuu wa nchi hizo mbili na matakwa ya zama mpya.

Huku akibainisha kuwa DPRK iko tayari kushirikiana na China ili kuimarisha urafiki wa kindugu kati ya nchi hizo mbili, Pak amesema DPRK itaendelea kuimarisha uratibu wa pande nyingi na China ili kulinda maslahi ya pamoja na amani na utulivu wa kikanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha