

Lugha Nyingine
Nchi za Kiarabu na Russia zakubaliana kuongeza ushirikiano (5)
![]() |
Mkutano wa 6 wa Baraza la Ushirikiano kati ya Nchi za Kiarabu na Russia ukifanyika mjini Marrakech, Morocco, Desemba 20, 2023. (Xinhua/Huo Jing) |
MARRAKECH, Morocco - Nchi za Kiarabu na Russia zimekubaliana siku ya Jumatano kuongeza ushirikiano katika masuala ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kushughulikia mgogoro wa Gaza, kwenye mkutano wa 6 wa Baraza la Ushirikiano kati ya Nchi za Kiarabu na Russia uliofanyika katika mji wa kusini mwa Morocco wa Marrakech.
Mkutano huo umewakutanisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (AL), akiwemo Sergey Lavrov wa Russia, pamoja na Hossam Zaki, Katibu Mkuu Msaidizi wa AL.
Kwenye mkutano huo, wajumbe walitoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kubeba jukumu kubwa zaidi katika kufikia usimamishaji mapigano kwenye ukanda huo.
Kwa mujibu wa Lavrov, msimamo wa Russia kuhusu suala la Gaza unaendana na ule wa nchi za Kiarabu, akiongeza kuwa Russia "inaendelea na juhudi zake za kuhakikisha utulivu wa muda mrefu wa uhusiano kati ya Israel na Palestina kwa msingi wa mfumo wa kisheria unaotambuliwa kimataifa."
Wajumbe hao pia wamejadili mada kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Nchi za Kiarabu na Russia, hasa katika nyanja za utamaduni, sayansi na nishati.
Likiwa lilianza Mwaka 2009, Baraza la Ushirikiano kati ya Nchi za Kiarabu na Russia limekua na kuwa jukwaa muhimu kwa nchi za Kiarabu na Russia kubadilishana mawazo na kuratibu misimamo kuhusu masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma