Meli kubwa ya kwanza ya safari ya kitalii inayoundwa na China yenyewe yatoka bandari na kufanya safari ya majaribio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2023
Meli kubwa ya kwanza ya safari ya kitalii inayoundwa na China yenyewe yatoka bandari na kufanya safari ya majaribio
Picha iliyopigwa tarehe 24, Desemba ikionesha muonekano wa ndani wa meli ya “Adora Magic City”.

Tarehe 24, Desemba, meli kubwa ya kwanza ya safari ya kitalii inayoundwa na China yenyewe, “Adora Magic City” imetoka bandari ya kimataifa ya meli za kitalii ya Shanghai Wusongkou ili kuanza safari yake ya kwanza ya majaribio.

Mabaharia karibu 1300 kutoka sehemu mbalimbali duniani wamepanda meli kwa ajili ya kutoa huduma kwa abiria wanaoshiriki na kukamilisha safari hiyo ya majaribio pamoja nao. Meli nzima itafanya kazi kwa ipasavyo katika hali ilivyo ya kama safari rasmi ili kupima uwezo wa uendeshaji na usimamizi wa meli.

Safari hiyo ya majaribio itamalizika tarehe 25, Desemba, halafu safari ya pili ya majaribio itaanza. Kwa kupitia majaribio hayo mawili, itahakikisha kuwa huduma bora zitatolewa kwa abiria katika safari yake rasmi ya kwanza ya tarehe 1, Januari, 2024.

Picha na Ding Ting/Xinhua

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha