Shule za msingi na za sekondari za maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi ya Wilaya ya Jishishan zarejesha masomo kwa utaratibu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 25, 2023
Shule za msingi na za sekondari za maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi ya Wilaya ya Jishishan zarejesha masomo kwa utaratibu
Picha na Jiumeidanzeng/Chinanews

Desemba 25, Shule ya Msingi ya Matumaini ya Yangshan katika Wilaya ya Jishishan ya Eneo linalojiendesha la kabila la Wahui la Linxia la Mkoa wa Gansu imerejesha masomo shuleni. Asubuhi ya siku hiyo, wanafunzi 76 wote walikuja shuleni na kushiriki kwenye hafla ya kupandisha bendera ya taifa saa mbili na nusu. Wanafunzi wote wakishirikishwa na walimu wao walijifunza ujuzi kuhusu “tetemeko la ardhi” na “njia za kukimbilia”, na kufanya mazoezi kwenye uwanja wa michezo.

Siku hiyo, shule za msingi na za sekondari katika Wilaya ya Jishishan zilirejesha masomo yao kwa utaratibu, na shule za msingi 152 zote za mahema kwa muda za wilaya ya Jishishan zilianza masomo pia. Walimu 1,136 wanafanya shughuli za mafunzo kwenye maeneo ya shule yaliyopangwa kwa muda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha