Kamati Kuu ya CPC yafanya kongamano la kuadhimisha miaka 130 tangu kuzaliwa kwa Mao Zedong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2023
Kamati Kuu ya CPC yafanya kongamano la kuadhimisha miaka 130 tangu kuzaliwa kwa Mao Zedong
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye kongamano lililofanywa na Kamati Kuu ya CPC kuadhimisha miaka 130 tangu kuzaliwa kwa Komredi Mao Zedong katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Desemba 26, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING - Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya kongamano kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing siku ya Jumanne asubuhi kukumbuka miaka 130 tangu kuzaliwa kwa Komredi Mao Zedong, ambapo Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama, alitoa hotuba muhimu katika kongamano hilo.

Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kusukuma mbele dhamira kuu iliyoanzishwa na Komredi Mao Zedong na kutoa wito kufanyika kwa juhudi za kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu zaidi na kulistawisha Taifa la China katika sekta zote kwa kutafuta maendeleo ya mambo ya kisasa ya China.

“Fikra Mao Zedong ni utajiri wa kiroho wenye thamani kwa Chama chetu na itaongoza hatua yetu kwa muda mrefu,” Rais Xi amesema, huku akisisitiza kwamba njia bora ya kumkumbuka Komredi Mao Zedong ni kuendelea kusukuma mbele mambo aliyoanzisha.

Katika hotuba yake, Rais Xi amesema maisha yote ya Komredi Mao Zedong ni yaliyokuwa yamejitoa kwa ajili ya ustawi wa taifa, ustawi na furaha ya watu na kwamba Mao aliwaongoza watu kwa hamasa kubwa kufuata Umaksi kwa kuendana na mazingira ya China, na kuunda Chama cha kikomunisti cha China kilicho kikuu, kitukufu na kisahihi na kuanzisha China Mpya huku watu wakiwa mabwana wa nchi.

Huku akieleza kuwa kazi kuu ya Chama kizima na taifa zima katika safari mpya ya zama mpya ni kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu zaidi na kulistawisha Taifa la China katika sekta zote kwa kutafuta maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, Rais Xi amesema ni dhamira kuu iliyorithishwa kutoka kwa wanamapinduzi wakongwe akiwemo Mao Zedong, na ni jukumu zito la kihistoria la Wakomunisti wa China ya leo.

Katika safari mpya, hatupaswi kamwe kusahau nia yetu ya awali na majukumu yetu, na lazima tubaki na kujiamini katika historia yetu na kufahamu juhudi za kihistoria, ili kuendeleza kwa kasi lengo kuu la maendeleo ya mambo ya kisasa ya China, amesema Xi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha