Mkutano wa mawasiliano ya ustaarabu kati ya China na Tunisia wafunguliwa Tunis

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2023
Mkutano wa mawasiliano ya ustaarabu kati ya China na Tunisia wafunguliwa Tunis
Ji Bingxuan, Mkuu wa Shirika la Mawasiliano ya Kimataifa la China, akizungumza kwenye mkutano wa mawasiliano ya utamaduni na ustaarabu kati ya China na Tunisia mjini Tunis, Tunisia, Desemba 25, 2023. (Xinhua)

TUNIS - Mawasiliano na Mazungumzo kuhusu ustaarabu kati ya China na Tunisia yataleta maendeleo na ustawi wa nchi hizo mbili, Mkuu wa Shirika la Mawasiliano ya Kimataifa la China (CAFIU) Ji Bingxuan amesema siku ya Jumatatu kwenye mkutano wa mawasiliano ya utamaduni na ustaarabu kati ya China na Tunisia uliofanyika huko Tunis, mji mkuu wa Tunisia, na kuhudhuriwa na watafiti, wasomi na wanahistoria wa China na Tunisia.

Akizungumza kwenye mkutano huo ulioandaliwa kwa pamoja na CAFIU na Taasisi ya Tunisia ya Urithi wa Taifa (INP), Ji amesema katika hotuba yake kwamba Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia lililotolewa na China linalenga kuishi pamoja na kufundishana kati ya ustaarabu mbalimbali, na linatoa mchango muhimu katika kuhimiza mchakato wa maendeleo ya kisasa ya jamii ya wanadamu na ustaarabu tofauti duniani.

Kwa upande wake Tarek Baccouche, Mkurugenzi wa INP, amesema kuwa ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Tunisia umeshuhudia kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, na mradi wa pamoja wa utafiti wa mabaki ya kale ya utamaduni wa China na Tunisia ulioanzishwa mwaka huu unaendelea vizuri.

Mwaka 2024 ni maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tunisia, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili utafikia kiwango cha juu zaidi, Baccouche amesema.

M'hamed Hassine Fantar, mwanahistoria wa Tunisia, alitambulisha kwa ufupi ustaarabu wa kale wa Tunisia kwenye mkutano huo, hasa historia ya Carthage.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha