Watu takriban 25 wafariki dunia kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Mashariki mwa DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 28, 2023
Watu takriban 25 wafariki dunia kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Mashariki mwa DRC
Picha iliyopigwa Desemba 27, 2023 ikionyesha watu wakiwa wamesimama kwenye nyumba zilibomolewa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha huko Bukavu, Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). (Str/Xinhua)

KINSHASA – Watu takriban 25 wamefariki baada ya mvua kubwa kunyesha Bukavu, Mji Mkuu wa Jimbo la Kivu Kusini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), usiku kucha siku ya Jumanne, ambapo televisheni ya taifa ya nchi hiyo, RTNC imetangaza kuwa miili ya watu imepatikana katika vitongoji kadhaa kote mjini humo, na nyumba zimesombwa na maji ya mvua huku ikieleza kuwa vifo vinatazamiwa kuongezeka pia.

Wiki iliyopita, watu takriban 20 walifariki dunia katika maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika Kijiji cha Kalingi katika Wilaya ya Mwenga, Jimbo la Kivu Kusini.

Mwezi Mei, mwaka huu wa 2023, katika eneo la Kalehe la Jimbo la Kivu Kusini, miili takriban 438 ilipatikana katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa. Serikali za mtaa zilikadiria kuwa watu zaidi ya 5,000 walikuwa bado hawajulikanai walipo.

Mafuriko na maporomoko ya ardhi ni ya kawaida nchini DRC wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza Mwezi Septemba hadi Mei, na mara nyingi huwa na athari mbaya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha