Mkutano wa Kazi ya Kamati Kuu ya Chama kuhusu mambo ya nje ya China wafanyika Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2023
Mkutano wa Kazi ya Kamati Kuu ya Chama kuhusu mambo ya nje ya China wafanyika Beijing
Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kazi ya Kamati Kuu ya Chama kuhusu Mambo ya Nje ya China. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Mkutano wa Kazi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu Mambo ya Nje ya China umefanyika Beijing kuanzia Jumatano hadi Alhamisi, ambapo Rais wa China Xi Jinping ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) alihudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu akifanya majumuisho kuhusu mafanikio ya kihistoria na uzoefu muhimu wa mambo ya diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalum wa China katika zama mpya.

Akiongoza mkutano huo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesisitiza kufanya vizuri mambo ya nje ya China katika safari mpya chini ya uelekezaji wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu Diplomasia, na ametoa matakwa ya kusoma na kutekeleza misingi ya hotuba muhimu ya Xi.

Mkutano huo umeeleza kwamba tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC, mafanikio ya kihistoria yamepatikana na mabadiliko ya kihistoria yametokea kwenye kazi ya mambo ya nje ya China katika safari kubwa ya kusukuma mbele mambo ya ujamaa wenye umaalum wa China katika zama mpya.

Mkutano huo umebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika mambo ya nje ya China kama vile kuanzisha na kuendeleza Fikra ya Xi Jinping kuhusu Diplomasia, kuonyesha umaalum, mtindo na maadili ya kipekee ya China katika diplomasia, kuhamasisha ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, kuhimiza kujenga muundo wa uhusiano kati ya pande zote ulio wa kuishi pamoja kwa amani, wa utulivu na wenye uwiano wa maendeleo, kupanua mpangilio wa kimkakati wa wenzi wa pande zote duniani, na kujenga mtandao mpana wa ushirikiano ulio wa sifa bora wa kimataifa, na mafanikio mengine mengi.

Mkutano huo umeeleza kuwa, uzoefu wa thamani mbalimbali umepatikana kwenye mambo ya diplomasia ya China katika zama mpya na kwamba ni muhimu kufuata kanuni zilizowekwa.

Kuhusu masuala makuu yanayohusiana na mustakabali wa binadamu na mwelekeo wa Dunia, mkutano huo umesisitiza kushikilia msimamo ulio wazi na thabiti, kukalia sehemu ya juu ya kufuata maadili ya kimataifa, na kushikamana na nchi na watu walio wengi katika Dunia nzima.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha