

Lugha Nyingine
Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Jishi katika wilaya iliyokumbwa na tetemeko la ardhi nchini China wahamia shule nyingine (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2023
Mamia ya wanafunzi wa kidato cha tatu kutoka Shule ya Sekondari ya Jishi katika Wilaya ya Jishishan iliyokumbwa na tetemeko la ardhi hivi karibuni wamesafirishwa hadi Shule ya Kazi za Ufundi ya Linxia katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Wahui la Linxia kuanza tena masomo siku ya Alhamisi. Kwa mujibu wa mpangilio wa idara ya elimu katika eneo hilo, wanafunzi wote wa kidato cha tatu katika wilaya hiyo watarejea masomoni katika maeneo mengine wiki hii.
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 lilitokea katika Wilaya ya Jishishan katika Eneo la linalojiendesha la Kabila la Wahui la Linxia mnamo Desemba 18.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma