Barabara Kuu mpya yaunganisha Mji wa Beijing na Eneo Jipya la Xiong'an nchini China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 29, 2023
Barabara Kuu mpya yaunganisha Mji wa Beijing na Eneo Jipya la Xiong'an nchini China
Picha hii ikionesha magari yakipita kwenye sehemu ya Beijing ya barabara kuu ya Beijing-Xiong'an, Desemba 28, 2023. (Xinhua/Zhang Chenlin)

BEIJING - Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China imesema, sehemu mpya ya Barabara Kuu inayounganisha Mji wa Beijing na Eneo Jipya la Xiong'an katika Mkoa wa Hebei, Kaskazini mwa China, ambayo inatarajiwa kupunguza muda wa kuendesha gari kati ya barabara kuu ya tano ya mzunguko kusini-magharibi ya Beijing na Eneo Jipya la Xiong'an hadi saa moja, imefunguliwa kwa matumizi ya umma siku ya Alhamisi, ikiashiria kukamilika kwa barabara kuu nzima.

Sehemu kuu ya barabara hiyo ina urefu wa takriban kilomita 97, ikijumuisha sehemu ya Mkoa wa Hebei yenye urefu wa kilomita 70 na sehemu ya Beijing yenye urefu wa kilomita 27.

Mwezi Aprili 2017, China ilitangaza mpango wa kuanzisha Eneo Jipya la Xiong'an, ambalo linajumuisha Wilaya za Rongcheng, Anxin, na Xiongxian na baadhi ya maeneo ya karibu.

Eneo hilo linalenga kuupunguzia Mji wa Beijing kazi zisizo muhimu kuhusiana na hadhi yake ya mji mkuu wa China, na wakati huo huo kuhimiza uratibu wa maendeleo ya eneo la Beijing-Tianjin-Hebei.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha