Miaka 60 ya Msaada wa Matibabu wa China Duniani: Hisani na moyo mwema vyajenga "Daraja la Afya”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2024
Miaka 60 ya Msaada wa Matibabu wa China Duniani: Hisani na moyo mwema vyajenga
Hii ni picha ya kumbukumbu ya Zhang Youming (kulia), daktari aliyekuwa wa timu ya kwanza ya madaktari wa China iliyotumwa nchini Algeria kutoa msaada wa matibabu. Zhang mwenye umri wa miaka 90 kwa sasa alifanya kazi huko kwa miaka miwili na nusu, ambapo alifanikiwa kufanya upasuaji kwa zaidi ya elfu moja na kuwawezesha watoto wengi kuzaliwa salama. (Picha kwa hisani ya mhojiwa/Xinhua)

Mnamo mwezi wa Aprili, 1963, timu ya kwanza ya madaktari wa China ilitumwa nchini Algeria ya Kaskazini mwa Afrika, tangu hapo China ilianzisha utoaji wa msaada wa matibabu katika nchi za nje, mpaka sasa utoaji msaada huo umefikia muda wa miaka 60. Katika miaka 60 iliyopita, China imepeleka madaktari karibu 30,000 kwenda katika nchi na maeneo 76, ambao wametoa huduma za matibabu kwa wagonjwa karibu milioni 300; ambapo China imeanzisha ushirikiano wa aina mbalimbali na hospitali 48 za nchi 43; na pia imeshirikiana na nchi husika kuanzisha vituo 25 vya matibabu ya magonjwa maalumu, na kuingiza mamia ya teknolojia...... Katika miaka 60 iliyopita, madaktari wa China wa awamu hadi awamu wamekwenda katika nchi mbalimbali wakiendelea kujitolea katika huduma za matibabu, wakitumia ustadi wao bora wa matibabu, wakitafsiri kwa uwazi moyo wa timu ya madaktari wa China wa “kutoogopa taabu, kujitolea bila kujali chochote, kufanya matibabu na kuokoa maisha, na kuonesha upendo usio na mipaka."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha