Eneo la kuteleza kwenye barafu la mita 521 lavutia macho ya watu kwenye Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2024
Eneo la kuteleza kwenye barafu la mita 521 lavutia macho ya watu kwenye Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin, China
Watalii wakifurahia kuteleza wakiwa wameketi kwenye kifaa cha kuteleza kwenye barafu katika Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China Januari 1, 2024. (Xinhua/Xie Jianfei)

Kati ya burudani mbalimbali zilizopo katika bustani hiyo, bila shaka sehemu ya kuteleza kwenye barafu kwa urefu wa mita 521 ilivutia zaidi macho ya watalii.

Mkoa wa Heilongjiang nchini China unaojulikana kwa kuwa na majira ya baridi kali na ya muda mrefu yenye mandhari nzuri ya barafu na theluji, umekuwa ni kivutio cha utalii kinachopendwa zaidi kwa utalii wa majira ya baridi nchini China, ukivutia watalii wengi kutoka ndani na nje ya China wakati wa mapumziko ya mwaka mpya. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha