Picha: Sanamu ya kale ya Farasi wa Shaba iliyohifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Mkoa wa Gansu, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2024
Picha: Sanamu ya kale ya Farasi wa Shaba iliyohifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho ya Mkoa wa Gansu, China
Picha hii iliyopigwa tarehe 27, Oktoba, 2023 ikionesha muonekano wa mbele wa sanamu ya zama za kale ya farasi wa shaba kwenye Jumba la Makumbusho la Mkoa wa Gansu mjini Lanzhou, Mji Mkuu wa Mkoa wa Gansu wa China.

Sanamu hiyo inayojulikana kwa jina maarufu la “Farasi wa Mwendokasi wa Kuruka wa Kukanyaga Ndege”, ilifukuliwa katika miaka 1960 kwenye Kaburi la Leitai la Enzi ya Han ya Mashariki ya China (B.K 25-220) mjini Wuwei, Gansu, na hivi sasa inahifadhiwia kwenye Jumba la Makumbusho la Mkoa wa Gansu. Sanamu hiyo ilikuwa alama ya utalii wa China mwaka 1983. (Xinhua/Wang Yuguo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha