

Lugha Nyingine
Algeria na Sierra Leone zaahidi kuimarisha juhudi za amani za kimataifa (3)
![]() |
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune (kulia) akimkaribisha Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio mjini Algiers, Algeria, Januari 3, 2024. (Ikulu ya Algeria/ Xinhua) |
ALGIERS - Algeria na Sierra Leone zimesisitiza siku ya Jumatano kujitolea kwao kushirikiana kwa karibu katika kudumisha amani na usalama wa kimataifa kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kati ya Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio aliyeko ziarani mjini Algiers na Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune.
"Kama nchi wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Algeria na Sierra Leone zimeahidi kulinda amani na usalama duniani kwa mujibu wa Katiba ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa." Rais Tebboune amesema.
Algeria na Sierra Leone zilichaguliwa kuwa nchi wanachama wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa muhula wa 2024-2025, kuanzia Januari 1 2024, hadi Desemba 31, 2025.
Rais Tebboune amesema nchi zote mbili zimetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kutambua kutotendewa haki kihistoria wanakokabaliana nako wapalestina, hasa katika Ukanda wa Gaza.
Aidha, viongozi wote wawili wameahidi kuimarisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na nishati, biashara, viwanda, kilimo, elimu, utafiti na uvuvi, na kujadili kuanzishwa kwa baraza la pamoja la biashara.
Kwa upande wake, Bio amesema kuwa mkutano kati yake na mwenzake wa Algeria ulikuwa "muhimu," ambapo walijadili masuala kuhusu maslahi ya pamoja na kukubaliana kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika ngazi zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma