Tarafa ya Shuihou yaendeleza nyumba za kuwapokea wageni na kuongeza huduma mbalimbali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2024
Tarafa ya Shuihou yaendeleza nyumba za kuwapokea wageni na kuongeza huduma mbalimbali
Picha hii iliyopigwa Januari 6, 2024 ikionyesha nyumba za kupokea wageni katika Tarafa ya Shuihou ya Mji wa Qianshan, Mkoa wa Anhui, Mashariki mwa China. (Xinhua/Du Yu)

Huduma ya kupokea watalii katika Tarafa ya Shuihou iliyoko chini ya Mlima Tianzhu ilikuwa ikiwapokea tu watalii waliokuja kutazama mandhari ya milimani. Lakini katika miaka ya hivi majuzi, huduma zimeongezeka kuwa za aina mbalimbali kutokana na maendeleo ya idadi kubwa ya nyumba za kupokea wageni zenye ubora wa juu. Biashara ya aina mpya ya "theluji jumlisha nyumba za wageni" pia imeanzishwa ili kuendana na eneo la mapumziko lililoko karibu la kuteleza kwenye theluji wakati wa majira ya baridi. Shughuli za utalii zinazofanywa kwenye msingi wa nyumba hizi za kuwapokea wageni na familia mbalimbali za wakazi zimetoa nafasi za ajira kwa wakazi zaidi ya 3,000 wa eneo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha