Chama tawala cha Bangladesh cha Awami League chashinda viti 223: Tume ya Uchaguzi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2024
Chama tawala cha Bangladesh cha Awami League chashinda viti 223: Tume ya Uchaguzi
Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina akizungumza kwenye mkutano mjini Dhaka, Bangladesh, Januari 8, 2024. (Ofisi ya Waziri Mkuu Bangladesh / Xinhua)

DHAKA - Chama tawala cha Bangladesh Awami League (AL) kinachoongozwa na Waziri Mkuu Sheikh Hasina kimeshinda viti 223 kati ya 298 katika uchaguzi wa wabunge nchini humo, Kamishna Mkuu wa Uchaguzi Kazi Habibul Awal alisema siku ya Jumatatu ambapo kati ya viti 300, matokeo ya jimbo moja la uchaguzi yamecheleweshwa. Wakati huo huo, upigaji kura katika jimbo moja la uchaguzi uliahirishwa kufuatia kifo cha mgombea huru.

Nchini Bangladesh, chama kinaweza kuunda serikali kama kitafanikiwa kunyakua viti 151 vya bunge kwa jumla.

Awal amesema kuwa idadi ya wapiga kura katika uchaguzi wa 12 wa bunge la Bangladesh ilifikia asilimia 41.8 ya jumla ya wapiga kura wote halali. Nchini Bangladesh, chama kinachopata viti vingi bungeni kinaweza kuunda serikali, ameongeza.

Wagombea zaidi ya 260 kutoka chama tawala cha AL walishiriki uchaguzi huo wa kitaifa. Upigaji kura ulianza saa 2:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 10:00 jioni kwa saa za huko siku ya Jumapili katika vituo zaidi ya 42,000 vya kupigia kura kote nchini humo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha