

Lugha Nyingine
Rais wa UAE na Blinken wasisitiza haja ya kuepuka kupanuka kwa mgogoro wa Gaza (2)
ABU DHABI - Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken siku ya Jumatatu wamesisitiza umuhimu wa kuepuka kupanuka kwa mgogoro wa Gaza katika kanda hiyo na kutafuta suluhu ya wazi ili kufikia utulivu wa kikanda ambapo pia kwenye mkutano wao katika mji mkuu wa UAE, Abu Dhabi, wamejadili uhusiano wa pande mbili na njia za kuuboresha ili kutumikia maslahi yao ya pamoja.
Vile vile wamegusia masuala kadhaa ya kikanda na kimataifa yanafuatiliwa na nchi hizo mbili na matukio katika eneo la Mashariki ya Kati hususan yale ya maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu na madhara makubwa ya mgogoro wa Ghaza katika masuala ya amani, utulivu na usalama wa eneo hilo.
Rais wa UAE amesisitiza haja ya kufanya juhudi kwa ajili ya usimamishaji wa vita katika Ukanda wa Gaza ili kulinda maisha ya raia, kuhakikisha kuanzishwa kwa mifumo ya kudumu na salama ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Ukanda huo bila vikwazo, na kuzuia wasilazimishwa kuhama makazi na maeneo yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma