

Lugha Nyingine
Miradi ya reli iliyojengwa na China yaleta safari za furaha za Msimu wa Sikukuu (Yuletide) nchini Nigeria
![]() |
Picha iliyopigwa Juni 10, 2021, ikionyesha mandhari ya nje ya Stesheni Mobolaji Johnson ya reli ya Lagos-Ibadan mjini Lagos, Nigeria. (Picha na Emma Houston/Xinhua) |
LAGOS - Wakipanda treni ya kuelekea Ibadan katika Stesheni ya Mobolaji Johnson huko Lagos, mji ambao ni kitovu cha uchumi cha Nigeria na wenye watu wengi zaidi, familia ya watu sita waliketi kwenye viti vyao katika behewa la daraja la pili, vicheko vyao vikijaza matajiro ya likizo ya Yuletide (msimu wa Krismasi).
Adeniyi Salaudeen, mwanamume wa makamo na baba wa familia, mwenye tabasamu, alieleza simulizi zake za sikukuu za Krismasi zilizopita na mke wake na watoto wake wanne huku wakistaajabishwa na behewa la kisasa walilokuwa ndani yake.
"Nimepata uzoefu huu hapo awali, nikisafiri kwa treni. Nimefurahia sana kusafiri," Salaudeen ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano huku king’ora cha treni kikipulizwa, kuashiria kuanza kwa safari ya kuelekea Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria.
Reli ya Lagos-Ibadan, ambao ni mradi mkubwa wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI) lililotolewa na China, ilijengwa na Shirika la Uhandisi na Ujenzi la China (CCECC) na inaunganisha miji ya kusini-magharibi ya Lagos, Abeokuta, na Ibadan. Reli hiyo ilianza kufanya kazi rasmi Mwaka 2021, ikirahisisha usafirishaji wa umma na usafirishaji wa bidhaa za mafuta nchini humo. Mradi huo ni reli ya kwanza nyembaba ya njia mbili kujengwa Afrika Magharibi.
"Nilipokuwa mdogo, nilisafiri mara nyingi kwa treni kati ya Abeokuta na Lagos. Nilisoma Abeokuta na wazazi wangu walikuwa Lagos. Wakati huo, huduma ya barabara ilikuwa mbaya sana kutokana na barabara mbovu," Pa Makanjuola Azeez mwenye umri wa miaka 90 amesema, wakati akikumbuka siku za zamani.
"Nimekuwa nikitumia huduma ya treni kwa muda kadhaa, lakini nilitaka watoto wangu wapate uzoefu. Ni likizo ya familia. Safari ni nzuri, haina shida yoyote, na pia ni haraka," ameongeza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma