

Lugha Nyingine
Ofisa katika Serikali ya Angola asema Chapa za magari za China zimeleta magari yenye ubora na ya bei nafuu nchini humo
LUANDA – Chapa za magari za China zinaleta magari yenye ubora wa juu na ya bei nafuu nchini Angola, amesema Amadeu Nunes, Waziri wa Mambo ya Biashara wa Angola, wakati akitoa hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa duka la kwanza la 4S la chapa ya magari ya China ya Great Wall (GWM), siku ya Jumatano, mjini Luanda, Angola.
Nunes amesema kuwa chapa nyingi zaidi za China nchini Angola zitaboresha soko la magari nchini humo, na kuleta ushindani zaidi na kuwapa wateja bidhaa bora na za bei nafuu.
"GWM, ikiwa ni chapa ya China, kwa mara nyingine tena inaonesha umuhimu wa urafiki wa karibu wa kibiashara kati ya nchi zetu, na ningependa kusisitiza kwamba China ni moja ya washirika wa kimsingi katika maendeleo yetu," amesema.
Joshwa Lourenco, mkuu wa mauzo wa GWM nchini Angola, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa bidhaa nyingi za China zipo katika soko la Angola na zinakubalika vyema na wateja.
"Kwa upande wa bei na ubora, bidhaa za China, kwa ujumla, tayari zimeonyesha matokeo mazuri katika soko la Angola," amesema.
GWM, kampuni ya China inayooongoza kwa magari ya matumizi ya michezo (SUV) na mtengenezaji wa magari madogo ya kubeba mizigo, imeingia rasmi katika soko la Angola kwa kuzindua duka lake la kwanza la 4S, huu ni muundo wa uuzaji wa magari, ambao unaunganisha mauzo, huduma, vipuri, na uchunguzi kuwa mnyororo mmoja, na kutoa huduma kwa pande zote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma