Uchaguzi wa urais waanza katika nchi ya Visiwa vya Comoro (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024
Uchaguzi wa urais waanza katika nchi ya Visiwa vya Comoro
Mtu akipiga kura kwenye kituo cha kupigia kura huko Mitsudje, Visiwa vya Comoro, Januari 14, 2024. (Xinhua/Wang Guansen)

Moroni – Nchi ya Visiwa vya Comoro imeanza duru yake ya kwanza ya uchaguzi wa rais siku ya Jumapili ili kumchagua kiongozi wake mkuu kutoka miongoni mwa wagombea sita, akiwemo Rais wa sasa Azali Assoumani, kwa miaka mitano ijayo ambapo kwa mujibu wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), wapiga kura 338,940 waliojiandikisha kati ya idadi ya jumla ya watu takribani 900,000 walikuwa wakitarajiwa kupiga kura katika vituo 868 kote nchini humo kuanzia saa 1asubuhi hadi saa 12 jioni kwa saa za huko.

Matumizi ya barabara nchini humo yalikuwa yamedhibitiwa vikali siku ya Jumapili, kuruhusu magari yenye vibali maalum pekee.

Matokeo ya awali yanaweza kutangazwa leo Jumatatu na tume ya uchaguzi nchini humo.

Kama hakuna mgombea atakayeshinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura, zote halali zilizopigwa, wagombea wawili wenye idadi kubwa zaidi ya kura wataendelea hadi duru nyingine, Februari 25.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha