Zanzibar, Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya mapinduzi (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024
Zanzibar, Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya mapinduzi
Wazanzibar wakipunga bendera kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar huko Zanzibar, Tanzania Januari 12, 2024. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)

Wazanzibar siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita walikusanyika kwenye Uwanja wa Amani Mpya, ili kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea Januari 12, 1964, na kusababisha kupinduliwa kwa Sultani wa Zanzibar na serikali yake hasa ya Waarabu na wanamapinduzi wenyeji wa Afrika wa kisiwa hicho.

Rais Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar, Tanzania alishiriki kwenye sherehe za maadhimisho hayo uwanjani, akiwa pamoja na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Makamu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua, na Waziri Mkuu wa Burundi Gervais Ndirakobuca pia walishiriki kwenye sherehe za maadhimisho hayo.

Kilele cha maadhimisho hayo kilifuata shughuli zilizofanywa kwa karibu mwezi mzima, zikiwemo pamoja na hafla zilizoendeshwa na viongozi za uanzishaji na uwekaji wa jiwe la msingi kwa miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi .

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha