Huduma za TV za kidijitali za China zawezesha kupatikana kwa matangazo ya Kombe la Afrika katika nyumba za wanavijiji wa Cote d'Ivoire

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2024
Huduma za TV za kidijitali za China zawezesha kupatikana kwa matangazo ya Kombe la Afrika katika nyumba za wanavijiji wa Cote d'Ivoire
Watu wakitazama mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwa usaidizi wa mradi wa TV wa satelaiti wa China katika Kijiji cha Yaou, Cote d'Ivoire, Januari 14, 2024. (Xinhua/Han Xu)

ABIDJAN - Maelfu ya watu wanaoishi katika maeneo ya mbali nchini Cote d'Ivoire na nchi nyingine za Afrika wanaweza kutazama mashindano mbalimbali wakiwa nyumbani wakati michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 (AFCON) ilipoanza Jumamosi, kutokana na huduma za matangazo ya moja kwa moja kutoka viwanjani zinazotolewa na StarTimes, Kampuni mwendeshaji wa televisheni za kidijitali ya China.

Mradi unaolenga kuunganisha vijiji 10,000 vya Afrika na huduma za televisheni za satelaiti ulipendekezwa wakati wa mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini, Mwaka 2015.

Hadi kufikia Desemba 2023, mradi huo unaotekelezwa na StarTimes, umesaidia vijiji 9,512 katika nchi 20 za Afrika kupokea mawimbi ya televisheni ya kidijitali. Kaya zaidi ya 190,000 zinanufaika moja kwa moja na mradi huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha