Uji wa "Laba" unaogawiwa bila malipo na Hekalu la Wenshu kwa ajili ya Sikukuu ya Laba wavutia watu Mjini Chengdu, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2024
Uji wa
Wakazi wakiwa wanechukua uji wa Laba.

Tarehe 16, Januari, shughuli ya “Kugawa Uji wakati wa Sikukuu ya Laba” bila malipo ilianza katika Hekalu la Wenshu lililopo Mji wa Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China. Uji wa Laba uliopikwa hapo hapo kwenye hekalu umevutia wakazi na watalii wengi kuja na kusubiri kwenye foleni.

Uji wa Laba unapikwa kwa kuwekwa vyakula mbalimbali ndani yake. Ni mlo wa kijadi wakati wa Sikukuu ya Laba ya China. Mwaka huu sikukuu hiyo itakuwa tarehe 18, Januari.

Hekalu la Wenshu ni hekalu maarufu la Kibudha lililojengwa zama za kale, na pia ni kivutio maarufu cha utalii. Shughuli hiyo ya kugawa uji itadumu kwa siku tatu na kutoa vikombe laki tatu vya uji wa Laba bila malipo.

(Picha/Liu Zhongjun)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha