Kuharakisha utengenezaji wa taa za jadi za China ili kukaribisha Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Rongjiang, Guizhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2024
Kuharakisha utengenezaji wa taa za jadi za China ili kukaribisha Mwaka Mpya wa Jadi wa China, Rongjiang, Guizhou
Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, wanakijiji wa Kabila la Wamiao katika Kijiji cha Bailie kilichoko Mji Mdogo wa Bakai katika Wilaya ya Rongjiang ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Watong, Mkoa wa Guizhou, Kusini Mashariki mwa China wana pilikapilika nyingi za kutengeneza taa za jadi za China ili kukidhi mahitaji ya soko la sikukuu.

Katika miaka ya hivi karibuni, Kijiji cha Bailie kilichoko Mji Mdogo wa Bakai katika Wilaya ya Rongjiang ya Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Watong, Mkoa wa Guizhou, Kusini Mashariki mwa China kimekuwa kikitegemea rasilimali nzuri za msitu ya mianzi kuelekeza na kuhamasisha wanakijiji kuendeleza shughuli za usukaji wa mianzi na kusaidia wanakijiji kutafuta ajira karibu na nyumbani na kuongeza mapato yao. (Picha na Li Changhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha