

Lugha Nyingine
Katika Picha: Watu wakisherehekea Siku ya Laba mjini Beijing, China (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 19, 2024
![]() |
Mkazi akionyesha bakuri la uji wa Laba kwenye Hekalu la Yonghegong mjini Beijing, China, Januari 18, 2024. (Xinhua/Chen Zhonghao) |
BEIJING –Kwa kufuata kalenda ya kilimo ya China, siku ya nane ya mwezi wa 12 ya kila mwaka, ni Siku ya Laba. Baada ya siku hiyo, wachina hasa wa kaskazini mwa China wanaanza kufanya maandalizi mbalimbali ya kukaribisha Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, au tuseme Sikukuu ya Spring. Katika Siku ya Laba, kuna mila na desturi ya kunywa uji wa Laba.
Uji wa Laba hutengenezwa kwa mchanganyiko wa aina mbalimbali za nafaka ikiwa ni pamoja na mchele wa kunatanata, maharage mekundu, mtama, uwele wa Kichina, njegere na mbegu kavu za mayunguyungi.
Wachina wanaamini kuwa mlo wa uji wa Laba kwa ajili ya siku hiyo una maana ya baraka kwa matarajio ya pamoja juu ya mavuno mengi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma