Safari ya magamba ya chaza kutoka pwani ya mashariki ya Afrika hadi China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2024
Safari ya magamba ya chaza kutoka pwani ya mashariki ya Afrika hadi China
Magamba ya chaza yaliyokandika kwenye kuta za nyumba yalitoka pwani ya mashariki ya Afrika. (Picha na Wang Jing/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Bandari ya Quanzhou iliitwa Bandari ya Citong katika zama za kale. Usafiri wa kirahisi baharini na ustawi wa biashara ya nje vilikuwa vimefanya Bandari ya Quanzhou kuwa "bandari kubwa ya kwanza ya Mashariki" wakati wa Enzi za Song na Yuan, na kusifiwa kuwa "Mji wa Mwangaza " katika maandishi ya Marco Polo.

Kutokana na ustawi wa biashara ya baharini, idadi kubwa ya meli za biashara za China zilizobeba hariri na vyombo vya kauri zilifunga safari kutoka Xunpu iliyoko kando ya kaskazini ya Bandari ya Quanzhou, zikisafiri kwa kufuata Bahari ya Hindi na kuelekea nchi za Asia Kusini, nchi za Kiarabu na nchi za Afrika Mashariki zilizoko pwanipwani.

Ukitembelea katika Kijiji cha Xunpu, unaweza kuona nyumba zilizojengwa kwa raslimali za mchanganyiko wa magamba ya chaza na matope ya baharini. Magamba hayo ya chaza yalitoka pwani ya mashariki ya Afrika.

Katika siku za zamani, wakati meli za biashara za China zilipokuwa zitakaporudi nyumbani baada ya kupakua bidhaa, wafanyakazi melini walikusanya magamba ya chaza kwenye pwani ya bahari na kuyaweka kuwa uwiano wa uzito kwenye meli. Magamba hayo ya chaza yaliyowasilishwa na kuachwa kwenye pwani ya Xunpu, ambayo ni vitu visivyoliwa, hivyo yalichukuliwa na wakazi wa huko kukandika kwenye kuta za nyumba zilizojengwa nao, na kuwa mtindo wa kipekee wa majengo ya pwani ya Kusini-Mashariki mwa China.

Mwaka 2022, ufundi wa kukandika magamba ya chaza kwenye kuta za nyumba wa Mji wa Quanzhou umeorodhishwa kwenye miradi wakilishi ya saba ya urithi wa mali ya utamaduni usioshikika ya Mkoa wa Fujian.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha