Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2024
Katika Picha: Maonyesho ya taa za kijadi ya bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, China
Watu wakitembelea maonyesho ya taa za kijadi ya Bustani ya Yuyuan mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Januari 21, 2024. (Xinhua/Liu Ying)

Huku Mwaka Mpya wa Jadi wa China ukikaribia, Bustani ya Yuyuan iliyoko mjini Shanghai, Mashariki mwa China imekuwa tena na mandhari ya sikukuu, ikiwa imepambwa na mamia ya taa za kuvutia za kijadi.

Maonyesho ya taa za kijadi ya Bustani ya Yuyuan ni kivutio kikuu cha kitamaduni mjini Shanghai wakati wa sherehe za Sikukuu ya Spring, au Mwaka Mpya wa Jadi wa China. Maudhui ya mapambo ya taa hizo za mwaka huu ni mwendelezo wa mwaka 2023 kuhusu "Maajabu ya Milima na Bahari," ambalo limehamasishwa na fasihi ya kale "Shan Hai Jing."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha