

Lugha Nyingine
Vibanio vya nywele vya maua kwa Wanawake wa Kijiji cha Xunpu cha China: Alama za utamaduni kwenye "Njia ya Hariri ya Baharini"
![]() |
Mwanamke wa Kijiji cha Xunpu anayevaa vibanio vya vywele vya maua. (Picha na Wang Jing/People's Daily Online) |
Kijiji cha Xunpu kipo kando ya pwani ya mashariki ya Mji wa Quanzhou katika Mkoa wa Fujian wa China kwenye mwambao wa Kaskazini wa Bandari ya Quanzhou, ambayo ni kituo cha kuanzia kwa Njia ya Kale ya Hariri ya Baharini.
“Si zawadi bila ya maua, hii ni mila na desturi ya watu wa Xunpu. Kutoa zawadi ya maua kunamaanisha kuwatakia heri na baraka, na kuvaa maua pia kunamaanisha kupata baraka,”amesema Zhuang Qun wa eneo la makazi ya Xunpu.
Katika zama za kale, wanawake wa Xunpu walianza kusuka nywele zao kwa mtindo wa gamba la konokono wa baharini wakiwa na umri wa miaka 12 au 13, na kuzibana kwa kutumia mifupa ya samaki katikati ya nywele. Waliweka vibanio viwili hadi vitatu vya nywele vilivyosukwa kwa maua karibu na kifundo na kuweka maua kadhaa ya hariri.
Wakati wa Enzi ya Song (B.K. 960-1279) na Enzi ya Yuan (B.K. 1271-1368) ya China ya kale, biashara za baharini zilistawi huko Quanzhou. Xunpu ilishuhudia pitapita za meli nyingi za wafanyabiashara zilizoacha alama za kihistoria za Njia ya Hariri ya Baharini.
“Katika zama za kale, mkuu wa mamlaka ya forodha ya Quanzhou alikuwa mfanyabiashara Mwarabu aliyeitwa Pu Shougeng. Alijenga ‘Bustani ya Yunlu” na kupanda maua yaliyoletwa kutoka nchi za kiarabu. Kati ya maua yaliyopandwa kwenye bustani hiyo, maua ya Jasminum grandiflorum yanatumika katika mila na desturia ya wanawake wa Xunpu ya kuvaa vibanio vya vywele vya maua” amefahamisha Zhuang.
Mnamo mwaka 2008, mila na desturia za wanawake wa Xunpu ikiwemo ya kuvaa vibanio vya nywele vya maua ziliorodheshwa kwenye urithi wa mali ya utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China.
Mpaka hivi leo, wanawake wa Xunpu bado wanafuata mila na desturia ya kuvaa vibanio hivyo vya nywele vya maua.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma