

Lugha Nyingine
Ofisa Mwandamizi wa Serikali ya Tunisia apongeza ushirikiano na China katika miaka 60 iliyopita
TUNIS – Katibu wa Nchi kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Uhamiaji na Watunisia wanaoishi Ng'ambo wa Tunisia, Mounir Ben Rjiba amepongeza ushirikiano mzuri kati ya nchi yake na China katika miongo sita iliyopita kwenye hafla ya kukaribisha maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tunisia siku ya Ijumaa jioni.
Amesema ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta za ujenzi wa miundombinu, matumizi ya rasilimali za maji na afya umewanufaisha wananchi wa Tunisia.
Amesema mkutano wa mafanikio kati ya viongozi wa China na Tunisia kwenye Mkutano wa viongozi wakuu wa China na nchi za Kiarabu uliofanyika katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh Mwezi Disemba 2022 umeainisha mwelekeo wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika siku zijazo.
Kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na ubalozi wa China nchini Tunisia huko Tunis, Balozi wa China nchini humo Wan Li amesema China ingependa kuimarisha ushirikiano na Tunisia katika nyanja mbalimbali, kujenga maelewano mapana zaidi, na kulinda kwa pamoja amani na maendeleo.
Ushirikiano wa kufuata hali halisi kati ya nchi hizo mbili umekuwa na matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia miaka 60 iliyopita, amesema balozi huyo wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma