Rais Xi na mwenzake wa Uzbekistan wafanya mazungumzo, wainua uhusiano kuwa wa kimkakati wa pande zote wa siku zote katika zama mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2024
Rais Xi na mwenzake wa Uzbekistan wafanya mazungumzo, wainua uhusiano kuwa wa kimkakati wa pande zote wa siku zote katika zama mpya
Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev na mkewe Ziroatkhon Mirziyoyeva katika Ukumbi wa Kaskazini wa Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo kati ya Xi na Mirziyoyev mjini Beijing, China, Januari 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev, wamefanya mazungumzo mjini Beijing siku ya Jumatano, na kutangaza kuendeleza uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa pande mbili wa siku zote katika zama mpya, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Uzbekistan yenye mustakabali wa pamoja kutoka mwanzo wa juu zaidi.

Rais Mirziyoyev yuko nchini China kwa ziara ya kiserikali.

Rais Xi ameeleza kuwa miaka 32 iliyopita, Uzbekistan ilikuwa nchi ya kwanza ya Asia ya Kati kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China. Na kwamba watu wa nchi hizo mbili wamefuata moyo wa Njia ya Hariri, na kuufanya urafiki kati ya China na Uzbekistan kukita mizizi na kuwa wenye nguvu.

Akisisitiza kwamba pande hizo mbili zimekuwa zikitendeana kwa udhati na kuaminiana, Rais Xi amesema nchi hizo mbili zinapaswa kusaidiana kithabiti zaidi katika kukabiliana na hali tata ya kimataifa iliyopo hivi sasa.

“China inaiunga mkono kithabiti Uzbekistan katika kulinda mamlaka ya nchi, uhuru na ukamilifu wa ardhi, na katika kuchagua njia yake ya maendeleo,” Rais Xi amesema, huku akitoa wito kwa mchango zaidi wa Kamati ya Ushirikiano wa Kiserikali na majukwaa mengine katika kuimarisha mawasiliano ya kimkakati na kuzidisha kwa pande zote hali ya kuaminiana kisiasa na kimkakati.

Amesema China ingependa kupanua ushirikiano na Uzbekistan katika mnyororo mzima wa viwanda vya magari yanayotumia nishati mpya na kushirikiana katika miradi mikubwa, ikiwa ni pamoja na umeme unaotokana na nishati ya jua, umeme unaotokana na nishati ya upepo na umeme unaotokana na nishati ya maji, kupunguza umaskini, kuunga mkono mkakati wa maendeleo ya uchumi wa kijani wa Uzbekistan na kuhimiza maendeleo endelevu.

Rais Xi pia amesisitiza uratibu na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kudumisha mwelekeo sahihi wa maendeleo ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), kutekeleza matokeo ya Mkutano wa viongozi wakuu wa China na Nchi za Asia ya Kati, kuimarisha mfumo wa China na Asia ya Kati, kuhimiza uongozi wa kimataifa na kikanda, na kuendeleza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake Rais Mirziyoyev amesema Uzbekistan ingependa kujifunza kutoka kwa uzoefu wa mafanikio wa maendeleo ya China na kufanya ushirikiano na China katika sekta mbalimbali.

Amesema nchi yake inafuata kwa uthabiti sera ya kuwepo kwa China moja, inapinga vikali uingiliaji wa nje katika masuala ya ndani ya China, na ingependa kutoa uungaji mkono kithabiti kwa China katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu ya China, ikiwa ni pamoja na Taiwan, Xinjiang na haki za binadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha