

Lugha Nyingine
China na Singapore zatia saini makubaliano ya kusameheana visa (4)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Septemba 8, 2023 ikionyesha bustani kando ya Ghuba ya Marina nchini Singapore. (Picha na Then Chih Wey/Xinhua) |
BEIJING - Wizara ya mambo ya nje ya China imesema kuwa, China na Singapore zimetia saini makubaliano ya kusahemeana visa mjini Beijing siku ya Alhamisi, ambayo yataanza kutekelezwa kuanzia Februari 9, ambapo sasa raia wa China na Singapore wenye pasipoti za kawaida wataruhusiwa kuingia na kukaa katika kila moja ya nchi hizi mbili bila visa kwa siku hadi 30.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Alhamisi amesema kuwa makubaliano hayo ambayo yataanza kutekelezwa usiku wa kuamkia Mwaka Mpya wa Jadi wa Dragoni wa China bila shaka ni zawadi ya mwaka mpya kwa watu wa nchi hizo mbili.
Amesema kuwa, itaongeza zaidi mawasiliano kati ya watu na kuendeleza uhusiano na ushirikiano kati ya China na Singapore katika nyanja mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma